Hati ya dharura
Unaweza tu kutumia hati ya dharura kusafiri safari moja kuelekea Tanzania. Huwezi kuitumia kurudi Uingereza.
Mahitaji ya Hati ya Dharura (ETD Checklist)
- Fomu ya Hati ya Dharura iliyojazwa kikamilifu
- Picha tatu (3) passport size
- Barua ya maombi ieleze udharura wa safari
- Ushahidi wa Uraia wa Tanzania wa mwombaji (Cheti cha kuzaliwa, Kopi ya Pasipoti ya Tanzania)
- Kama anayeombewa Hati ya Dharura ni mtoto ambaye hajawahi kupata Pasipoti. Ombi liambatanishwe na Cheti cha kuzaliwa mtoto pamoja na vivuli vya pasipoti za Wazazi
- Kama umepoteza Pasipoti, ombi la Hati ya Dharura ni lazima lifuate masharti yale yale ya maombi ya Pasipoti zilizopotea
- Ada ya Hati ya Dharura (ETD) ni £20.00
-
Bonyeza hapa kupata fomu ya ombi