TANGAZO

UHAKIKI WA WASTAAFU

Wizara ya Fedha na Mipango hivi karibuni ilifanya zoezi la kuhakiki wastaafu wote wanaolipwa pensheni na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Wastaafu ambao hawakujitokeza kuhakikiwa waliondolewa katika daftari la pensheni pamoja na kusitishwa malipo yao.

Wastaafu wote ambao hawakufanyiwa uhakiki kutokana na kuishi nje ya nchi, mnaombwa kufika katika ofisi za Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hapa London kwa ajili ya kufanyiwa uhakiki.

Mnaombwa kufika mkiwa na nyaraka zifuatazo;

  •  Kivuli cha kitambulisho cha mstaafu
  •  Kivuli cha Barua ya Tuzo
  •  Kivuli cha ATM card au Bank statement ( akaunti inayotumika kupokea malipo ya pensheni)
  •  Nakala ya malipo yoyote (payment voucher) ambayo umeshawahi kulipwa na Wizara.
  •  Nakala ya barua ya kuajiriwa au kuthibitishwa kazini.
  •  Kitambulisho cha Jeshi kwa Wanajeshi
  •  Nakala ya barua ya kustaafu au kustaafishwa.

Uhakiki utakuwa unafanyika siku za Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa 10:00am hadi 02:00pm.

Anwani ya Ubalozi:

3 stratford Place

London

W1C 1AS

Nambari ya Simu: 02075691470

Barua pepe: balozi@tanzaniahighcommission.co.uk