F. Eligibility:
- Pasipoti zinatolewa kwa Raia wa Tanzania tu. Hazitolewi kwa mwombaji ambaye anao urais wa nchi nyingine zaidi ya Tanzania.
- Raia wa Tanzania ambaye amepata uraia wa nchi nyingine hana budi kurejesha pasipoti ya Tanzania Ubalozini kwa ajili ya kufutwa.
- Pasipoti za Tanzania hazitolewi pia kwa watu wenye hadhi ya Ukimbizi.
- Mtoto mwenye Uraia Pacha anaweza kupewa pasipoti ya Tanzania ikiwa hana pasipoti za nchi nyingine zaidi ya Tanzania.
NB: Waombaji wa pasipoti za Tanzania WANATAKIWA kusoma maelezo muhimu yanayohusu utoaji wa pasipoti kwenye FOMU Ukurasa wa 3 na 4.