MAOMBI YA PASIPOTI

Ubalozi wa Tanzania Nchini Uingereza na Jamhuri ya Ireland unapenda kuwaarifu  Watanzania wote wanaoishi Uingereza na Jamhuri ya Ireland kuwa, Ubalozi umeanza kushughulikia maombi ya Pasipoti za kielektonic kuanzia tarehe 01/04/2019. Pasipoti za zamani zitaendelea kuwa na matumizi hadi ifikapo tarehe 31 January,2020,

 

E-PASSPORT APPLICATION

hii itamwondolea usumbufu wa kwenda Ubalozi kuchukua fomu ya maombi ya pasipoti, na badala yake ataipata na kuijaza fomu hiyo mtandaoni. Aidha, itasiaidia katika kuimarisha utunzaji wa kumbukumbu.

Huduma hii itamwondolea usumbufu wa kwenda Ubalozi kuchukua fomu ya maombi ya pasipoti, na badala yake ataipata na kuijaza fomu hiyo mtandaoni. Aidha, itasiaidia katika kuimarisha utunzaji wa kumbukumbu.

VIELELEZO VINAVYOHITAJIKA WAKATI WA UJAZAJI WA FOMU YA MAOMBI YA PASIPOTI

 1. Cheti cha Kuzaliwa Mwombaji

 2. Cheti/Kiapo cha Kuzaliwa Mzazi wa Mwombaji

 3. Picha 3 za Mwombaji za hivi karibuni

 4. Ada ya Fomu $15 na ada ya pasipoti $75

 5. Ushahidi wa ukaazi(viza).

 6. Kivuli cha pasipoti

 7. Barua ya maombi ya pasipoti

 

JINSI YA KUJAZA FOMU YA MAOMBI YA PASIPOTI

 1. Bofya Anza kujaza fomu, kwa Ombi Jipya
 2. Bofya ENDELEA ili kuendelea na Ombi ambalo halikufikia mwisho.
 3. Jaza Taarifa zako sahihi kwa ukamilifu
 4. Hifadhi Namba yako ya Utambulisho (Application ID) kwa matumizi ya baadaye.
 5. Jaza Taarifa za Pasipoti ya zamani (ikiwa uliwahi kuwa na pasipoti)
 6. Jaza Taarifa za Wadhamini na Watu ambao ungependa wapewe taarifa endapo utatakewa na tatizo lolote
 7. Ambatanisha Vielelezo vyote vinavyohitajika (kwa kuzingatia maelekezo)
 8. Hakiki Taarifa zako zote na kisha bofya kukubaliana nazo ikiwa ziko sahihi
 9. Lipia fomu yako baada ya kupatiwa Namba ya Kumbukumbu ya Malipo (Control Number)
 10. Chapisha “Print” ombi lako
 11. Omba miadi “Book appointment” kwa barua pepe passport@tzhc.uk . Ambatanisha jina lako lote,nambari ya simu na  nambari ya ombi “application ID” yako.
 12. Ukishatuma tafadhari subiri kupata mawasiliano kwa njia ya simu kutoka Ubalozini.

HAKIKISHA UNAPOKUJA UBALOZINI UMETIMIZA NYARAKA ZAKO KAMA IFUATAVYO:-

Note: Counsular services hours of operation 10:00am to 12:30pm and 2:00pm to 3:30pm.

Click here for  Online Passport Form