Utaratibu wa Malipo (Payment methods)
- Utaratibu wa Malipo:
- Malipo ya Fomu ya Pasipoti:
- Malipo ya fomu ya pasipoti ya £5.00 yanaweza kulipiwa kwenye kaunta yetu hapa Ubalozini kwa kutumia KADI;
- Kwa wale ambao hawawezi kufika Ubalozini malipo ya £5.00 yatafanywa kwa postal order ambapo mwombaji pia atatakiwa alete bahasha yenye anuani yake iliyobandikwa stempu za rejista ili apelekewe fomu; na
- Kwa waombaji wanaoishi Ireland, malipo ya £5.00 ya fomu yatafanywa kwa Bank draft, ambapo pia atatakiwa alete bahasha yenye anuani yake pamoja na Bank draft ya £6.00 kwa ajili ya stempu ili apelekewe fomu hiyo (£5.00 ya fomu na £6.00 ya stempu zote pamoja zinaweza zikawa kwenye Bank draft moja ya jumla ya £11.00).
Malipo ya Ada ya Pasipoti:
- Kwa KADI kwa wale wanaofika kwenye kaunta zetu.
- Kwa BANK TRANSFER – Barclays Bank
Sort Code: 20-71-74
Account No: 33205932
- Kwa BANK DRAFT kwa wanaoishi Jamhuri ya Nchi ya Ireland.