JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MAMBO YA NDANI  YA NCHI

IDARA YA UHAMIAJI

TAARIFA KWA UMMA

PASIPOTI ZA KI-ELEKRONIKIA

Idara ya Uhamiaji imeanza kutoa Pasipoti mpya za ki-elektronikia kwa watanzania kuanzia tarehe 31/1/2018, Pasipoti za zamani zitaendelea kuwa na matumizi hadi ifikapo tarehe 31 January,2020, Utaratibu mpya wa maombi kwa sasa utawahusu waombaji wa Pasipoti waliopo ndani ya nchi tu.
kwa waombaji waliopo nje ya nchi wataendelea na utaratibu wa zamani na kupewa pasipoti za zamani mpaka hapo mitambo ya kuchukua alama za vidole zitakaposimikwa kwenye Balozi zetu.
Asante.

Online Passport Form 

Hii ni huduma mpya inayomuwezesha muombaji kujaza Fomu ya Maombi ya Pasipoti kwa njia ya Kielektroniki kutokea popote alipo, Baada ya kujaza fomu hiyo mtandaoni na kuambatisha viambato vyote kama alivyoelekezwa mtandaoni, atatakiwa kuichapisha (Print) fomu hiyo na kufika nayo katika Ofisi ya Ubalozi iliyo karibu naye kwa ajili ya kushughulikiwa maombi yake ya Pasipoti.

Huduma hii itamwondolea usumbufu wa kwenda Ubalozi kuchukua fomu ya maombi ya pasipoti, na badala yake ataipata na kuijaza fomu hiyo mtandaoni. Aidha, itasiaidia katika kuimarisha utunzaji wa kumbukumbu.

PASSPORT HOURS OF OPERATION

Passport application services:              Monday to Friday from 10.00 am to 12.30 pm.

Passport collection:                                  Monday to Friday from 10.00 am to 12.30 pm and                                                                                                                                  02.00 pm noon to 03.30 pm.

Maombi Ya Pasipoti Maelezo Kwa Lugha Ya Kiswahili Tafadhari Bofya Hapa.

Tanzania Passport Application Information In English