Wizara ya Fedha na Mipango hivi karibuni ilifanya zoezi la kuhakiki wastaafu wote wanaolipwa pensheni na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Wastaafu ambao hawakujitokeza kuhakikiwa waliondolewa katika daftari la pensheni pamoja na kusitishwa malipo yao.
Wastaafu wote ambao hawakufanyiwa uhakiki kutokana na kuishi nje ya nchi, mnaombwa kufika katika ofisi za Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hapa London kwa ajili ya kufanyiwa uhakiki.
Mnaombwa kufika mkiwa na nyaraka zifuatazo;
Kivuli cha kitambulisho cha mstaafu
Kivuli cha Barua ya Tuzo
Kivuli cha ATM card au Bank statement ( akaunti inayotumika kupokea malipo ya pensheni)
Nakala ya malipo yoyote (payment voucher) ambayo umeshawahi kulipwa na Wizara.
Nakala ya barua ya kuajiriwa au kuthibitishwa kazini.
Kitambulisho cha Jeshi kwa Wanajeshi
Nakala ya barua ya kustaafu au kustaafishwa.
Uhakiki utakuwa unafanyika siku za Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa 10:00am hadi 02:00pm.
Viongozi wa Jumuiya za Watanzania kwenye maeneo waliopo wanaombwa kuleta taarifa zao (majina, simu, na email) Ubalozini ili tukamilishe ukurasa unaohusika.
Kuanzia tarehe 4 January 2016 malipo ya huduma zinazotolewa na Ubalozi kama vile visa, kubadili passport n.k. yatafanyika kwa njia ya kadi malipo au moja kwa moja kwenye benki ya Ubalozi. Fedha taslimu hazitapokelewa tena. Kwa wale wanaotuma maombi yao kwa njia ya posta, malipo yafanyike kupitia Barclays Bank; Akaunti nambari 13494241; Sort Code 20-71-74.

Copyright © 2021 Tanzania High Commission.