Ubalozi umepokea taarifa toka Benki ya Amana, Tanzania kuwa Benki hiyo imeanzisha akaunti maalum kwa ajili ya Diaspora. Akaunti hiyo inayojulikana kwa jina la Kilimanjaro Diaspora Account inaendeshwa kwa kufuata miongozo ya dini ya Kiislam (Sharia Compliance: Al Wadiah na Mudharabah contracts).

Benki hiyo imeomba ofisi za balozi zote za Tanzania zitumike kuthibitisha nyaraka za kufungulia Akaunti (verification of documents) zinazowasilishwa na watanzania waishio maeneo husika ya uwakilishi kabla ya kuendelea na taratibu zingine za kufungua Akaunti hiyo.

Maelezo zaidi kuhusu Akaunti hiyo yanaweza kupatikana kwenye tovuti ya Benki hiyo www.amanabank.co.tz au kwa simu namba +255222129007. Aidha kwa yeyote atakayehitaji anaweza kuongea moja kwa moja na Bw. Dassu Musa, Meneja wa Masoko na Miradi kwa namba +255786687832 au Bw. Muhsin Muhammed, Mkuu wa Kitengo cha Uzalishaji na Sharia kwa namba +255653283636.