Ubalozi unawatangazia Watanzania wote wenye uraia wa Tanzania kuwa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imeanzisha utaratibu wa kutoa huduma kwa haraka (fast track) ya utambuzi na usajiri kwa watakaokwenda nyumbani.

Ili kufanikisha zoezi hilo, Mamlaka imemteua Bi Rose Mdami kuwa Afisa Dawati atakayeshughulikia masuala ya Diaspora ndani ya Mamlaka ya NIDA. Dawati hilo litakuwa katika jingo la Magereza lililopo kwenye Barabara ya Kivukoni, jijini Dar es salaam.

Kutokana na changamoto zinazo zinazokabili mamlaka hiyo, kwa sasa NIDA haitowekza kufanya zoezi la utambuzi na usajiri nje ya nchi. Tunaomba wananchi hao kufika ofisi hiyo ili kupata huduma ya fast track pindi watakapokuwa Tanzania.