Masaa ya kazi
Huduma za kuchukua alama za vidole Jumatatu hadi Ijumaa 10:00 Asubuhi – 12:30 Mchana
Uchukuaji wa pasipoti mpya Jumatatu hadi Ijumaa 10:00 Asubuhi – 12:30 Mchana
02:00 Mchana – 03:30 Mchana
Maombi ya pasipoti yafanyika kwa “appointment”. Ili kupanga tarehe ya kuja kuchukuliwa alama za vidole tafadhari bofya hapa.
A. Mahitaji:
- Fomu ya pasipoti (CT 5) iliyojazwa kikamilifu kwenye vipengele vyote.
- Picha tano (5) za pasipoti zenye “background” ya rangi ya “blue” au rangi ya maji ya bahari. (Ziwe za hivi karibuni).
- Kivuli cha pasipoti ya zamani ukurasa 1 na ukurasa wenye picha na taarifa muhimu za muombaji (bio-data page).
- Kivuli cha kibali cha makazi au Visa.
- Kivuli cha cheti cha kuzaliwa/kiapo cha kuzaliwa cha mwombaji.
- Kivuli cha cheti cha kuandikisha uraia wa Tanzania wa mwombaji.
- Deed Poll ya badiliko la majina kwa wanaotaka kubadili jina.
- Kivuli cha cheti cha ndoa kwa wanaotaka kubadilisha jina kwa sababu ya ndoa.
Kama pasipoti imepotea au kuibiwa ni lalzima kuleta:-
- Loss report
- Maelezo binafsi kwa maandishi kueleza yafuatayo:
- Taarifa za pasipoti iliyopotea kwa maana ya Namba ya pasipoti, tarehe na mwaka ilipotolewa na DN yako;
- Mazingira ya kupotea/kuibiwa kwa pasipoti; na
- Mahali na tarehe ya kupotea/kuibiwa kwake.
- Tangazo la gazeti kuhusu kupotea/kuibiwa kwa pasipoti hiyo.
Malipo ya maombi ya Pasipoti (Passport Application fees)
- Utaratibu wa Malipo:
- Malipo ya Fomu ya Pasipoti:
- Malipo ya fomu ya pasipoti ya £5.00 yanaweza kulipiwa kwenye kaunta yetu hapa Ubalozini kwa kutumiaKADI;
- Kwa wale ambao hawawezi kufika Ubalozini malipo ya £5.00 yatafanywa kwa postal order ambapo mwombaji pia atatakiwa alete bahasha yenye anuani yake iliyobandikwa stempu za rejista ili apelekewe fomu; na
- Kwa waombaji wanaoishi Ireland, malipo ya £5.00 ya fomu yatafanywa kwa Bank draft, ambapo pia atatakiwa alete bahasha yenye anuani yake pamoja na Bank draft ya £6.00 kwa ajili ya stempu ili apelekewe fomu hiyo (£5.00 ya fomu na £6.00 ya stempu zote pamoja zinaweza zikawa kwenye Bank draftmoja ya jumla ya £11.00).
Malipo ya Ada ya Pasipoti:
- Kwa KADI kwa wale wanaofika kwenye kaunta zetu.
- Kwa BANK TRANSFER – Barclays Bank
Sort Code: 20-71-74
Account No: 33205932
- Kwa BANK DRAFT kwa wanaoishi Jamhuri ya Nchi ya Ireland.
Utaratibu wa Malipo (Payment methods)
Utaratibu wa Malipo:
- Malipo ya Fomu ya Pasipoti:
- Malipo ya fomu ya pasipoti ya £5.00 yanaweza kulipiwa kwenye kaunta yetu hapa Ubalozini kwa kutumiaKADI;
- Kwa wale ambao hawawezi kufika Ubalozini malipo ya £5.00 yatafanywa kwa postal order ambapo mwombaji pia atatakiwa alete bahasha yenye anuani yake iliyobandikwa stempu za rejista ili apelekewe fomu; na
- Kwa waombaji wanaoishi Ireland, malipo ya £5.00 ya fomu yatafanywa kwa Bank draft, ambapo pia atatakiwa alete bahasha yenye anuani yake pamoja na Bank draft ya £6.00 kwa ajili ya stempu ili apelekewe fomu hiyo (£500 hya fomu na £6.00 ya stempu zote pamoja zinaweza zikawa kwenye Bank draft moja ya jumla ya £11.00).
Malipo ya Ada ya Pasipoti:
- Kwa KADI kwa wale wanaofika kwenye kaunta zetu.
- Kwa POSTAL ORDER au BANK DRAFT kwa wanaoishi Ireland.
- Kwa BANK TRANSFER.
Muda wa kushughulikia maombi ya Pasipoti:
Eligibility:
- Pasipoti zinatolewa kwa Raia wa Tanzania tu. Hazitolewi kwa mwombaji ambaye anao urais wa nchi nyingine zaidi ya Tanzania.
- Raia wa Tanzania ambaye amepata uraia wa nchi nyingine hana budi kurejesha pasipoti ya Tanzania Ubalozini kwa ajili ya kufutwa.
- Pasipoti za Tanzania hazitolewi pia kwa watu wenye hadhi ya Ukimbizi.
- Mtoto mwenye Uraia Pacha anaweza kupewa pasipoti ya Tanzania ikiwa hana pasipoti za nchi nyingine zaidi ya Tanzania.
NB: Waombaji wa pasipoti za Tanzania WANATAKIWA kusoma maelezo muhimu yanayohusu utoaji wa pasipoti kwenye FOMU Ukurasa wa 3 na 4.